Available courses

Nikiongozwa na uzoefu wangu wa kujitolea, nilitaka kuhadithia watu wengine kote duniani kuhusu baadhi ya masuala ya shughuli hii ya kipekee na jinsi inaweza kubadilisha maisha ya mtu kwa namna ya maana na inayo dumu kwa muda mrefu. Kujitolea huwa na furaha na nafuu na kwa wakati mwingine huwa chombo cha changamoto kitakachokusaidia na kuwasaidia wengine. Katika kila jamii, kila mtu ana njia ya kipekee ya kuona na kuweza kujitolea. Unapofikiria jinsi ya kuwa mtu anayejitolea au ikiwa wewe ni mfanyakazi kijana ambaye angependa kueneza maarifa ya kujitolea kwako kwa watu ambao wangependa kujitolea, kozi hii itakupa taarifa wazi ya jinsi shughuli hii inaweza kuwa ya kuhusisha na kuwa wazi kwa kila mtu.

Sasa ni wakati wa kugundua kiini cha kujitolea pamoja!

Kila nitazamapo runinga au kurambaza mtandao wa kijamii ama kuskiza redio, mimi huzidiwa na kuishiwa na nguvu kwa sababu ya dhoruba ya habari mbaya ziangazavyo kwa vyombo vya habari. Huenda pia wewe huhisi jinsi nihisivyo, au sivyo? Miaka michache iliyopita, niliamua kupingana na dhoruba hii na kutafuta jinsi bora za kukumbana na shida tofauti na kuleta mabadiliko mema kwangu na kwa jamii yango. Njia moja bora ya kuleta mabadiliko kwa jamii ni utetezi!

Somo hili litakufunza aina za utetezi na jinsi ya kuzitumia kwa kiufupi ili uweze kuleta mabadiliko ulipo. Somo hili pia litakusaidia kuelewa mazingira mbalimbali ambamo utetezi unaweza leta mabadiliko. Pia utapata maarifa ya jinsi ya kufanikisha utetezi wako na kuufanya uvutie kwa watu unao walenga. Ni muhimu kujua kwamba somo hili pekee halikufanyi mtaalamu wa utetezi ila tu kwa uzoefu binafsi. Hata hivyo, somo hili litakurahisishia na kukupa mawaidha na mifano bora ya kuanzisha kampeni yako ya utetezi kupitia mitambo ya kjamii, kuandika sera njema na kupitisha kauli zako kuu kwa njia inayovutia na kuhamasisha.

Kwa kila siku na kila wakati wetu wa maisha, kuna kujitolea kupya. Ungana nami katika mada hii ili ujue zaidi jinsi ya kujiamini, kujitegemea, heshima na ufaafu wako. Jinsi ya kujiwezesha na kuwezesha wengine katika jamii yako.

Kozi inawalenga wale wakubwa (zaidi ya miaka kumi na nane) ambao hawana uzoefu na uwezeshaji maishani mwao au katika jamii. Hakuna masomo yanayohitajika au uhitimu wa masomo ya ngazi za juu. Fikira za ubunifu zitachangia pakubwa.

Je, umewahi kuhisi kama wewe pekee kwa sayari nzima ndiye tu anayepitia shida fulani? Je, umewahi kuwa na mawazo kuwa wewe pekee ndo mwendawazimu anayejaribu kubadilisha dunia? Ikiwa ni hivyo, msaada wa rika ndo mkakati mwafaka kwako. Kozi hii itakupa kiini cha maudhui hii ya msaada wa rika na jinsi unavyoweza kukufaidi wewe au jamii yako. Utasoma kuhusu aina za miundo ya msaada wa rika na mbinu za mawasiliano zenye ufanisi ambazo zitakuwezesha kuanzisha miundo ya msaada wa rika utakaofaa walengwa wako. Lakini kozi hii itakupa fursa ya kushiriki katika aina kadhaa za msaada wa rika zilizo kwa mtandao pamoja na wanaoleta mabadiliko duniani kote kujadili changamoto na kupaa msukumo mpya wa kuendelea na kazi yako na nguvu na motisha.

Kozi hii ya mtandao itakupa fursa maalum ya kupata vidokezo kutoka kwa Yoshimi Horiuchi, mfaniski katika kuleta mabadiliko ambaye ameweza kupata fedha za mradi wake wa kijamii. Kwa sasa ni msimamizi wa shirika la Always Reading Caravan, shirika la kijamii lenye wafanyi kazi wanane na zaidi ya maelfu ya walengwa kila mwaka mle kaskazini mwa Uthai.

Kupitia video tano fupi, utaweza kusoma siri zote za Yoshimi za kuchanga pesa kwa ufanisi zikiwemo: fedha za kuanzisha, kuweka alama ya biashara, mawasiliano, ufanisi wa kuathiri jamii na uendelevu. Pia utaweza kuhusiana na Yoshimi na wanaoleta mabadiliko ya ufanisi ili wasome mengi zaidi na kuhadithia wengine uzoefu wako!

Jiunge na kozi hii ikiwa unaanzisha mradi wa kijamii (au unapanga kuanzisha) na unahitaji kuchanga fedha zaidi!

"Utamaduni ni mara nyingi zaidi chanzo cha migogoro ya umoja. Tofauti za kitamaduni ni kero kwa bora na mara nyingi maafa" (G. Hofstede)

Mazungumzo kuhusu mtindo wa maisha ya wanajamii inazidi kupata umuhimu kadri muingiliano unavyozidii kufanyika duniani haswa katika utendaji kazi na mazingira yake. Watu katika mataifa/nchi mbalimbali hujifunza tabia ya jumuia na mtindo mbalimbali/ anwai ya mazungumzo. Uwezo wa kujifunza jinsi jamii mbalimbali zinavyozungumza imekuwa jambo la kuangaziwa katika dunia ya sasa.

Mashirika mengi ya kisasa yanafanya kazi kotekote ulimwenguni, hivyo basi waajiri na waajiriwa, wanapaswa kujifunza jinui ya kuzungumza na washirika wao, wafanyakazi wenzao na pia waajiriwa kutoka katika jamii zingine. Aidha mashirika pia yanafaa kujua jinua ya kuzungumza na washiriki wao na wale wanaojitolea kutoka kwa jamii mbalimbali, kwa sababu ujumbe wenye maana/ umuhimu unaweza potea wakati wa kutafsiri, hivyo basi kutela kuchanganyikiwa na aibu.

Kozi hii inakutanguliza katika vipengele muhimu kuhusu mtindo wa mazungumzo wa jamii. Inalenga kupeana mtizamo mpya kuhusu jamii mbalimbali na mambo muhimu kuyahusu. Pia inaweza kuwa mwanzo wa safari yako kuhusiana na mitindo ya jamii. Pamoja nawe umepewa mwaliko wa kuandamana na marafiki zako, waajiriwa wenzako na wasaidizi wako.

Kozi hii ina mada kadha ambazo hupatikana kila wakati. Unatakiwa kuyapitia (mada hizo) ukiwa mtu binafsi na kufanya kazi iliyomo.

Hakuna walimu wa kibinafsi au wasimalizi wa kozi hii lakini waweza kuuliza maswali kuhusiana na huduma hii forum. Waweza kuichukua na kuifanya kozi/kozi hii mkiwa timu au ukiwa pekee yako.

Kozi ya kubuni wa masomo ya elektroniki iko na sehemu nane ambazo zitakuanzishia dhana za jinsi ya kuhusisha washiriki wako kwa masomo yanayotapikana kwenyemazingira ya masomo ya mtandao. Pia, kozi hii itakuonyesha njia na mbinu tofauti za kutengeneza na kubuni maudhui ya masomo ya kozi za mtandaoni ambayo ni ya kisasa na inaridisha. Kozi hii imetengenezwa ili ifikie walio wapya kwa kubuni maudui ya masomo ya elektroniki na kwa hivyo hakuna uzoefu mwingine unaohitajika.

Kwa wale wote wataweza kumaliza zoezi saba kwa zote tisa tutawapa karatasi la onyesho la ukamilisho.

Kozi hii yatupa fursa ya kipekee ya vijana wafanyi kazi na wengine ile wapate kuelewa kwa kina , elimu ya vitendo na ujuzi wa kushirikiana na kuingiliana na watu walio na ulemavu na watu waliotengwa kwa kutumia hisia-mwenzi na ufahamu mwema wa maisha na hali zao. Kozi hii imebuniwa ili kukabiliana na uhamasishaji wa watu walio na ulemavu. Kuna watu wengi walio na mahitaji tofauti ambao wanapitia changamoto nyingi katika jamii. Shughuli na vifaa vya mafunzo yetu zimebuniwa kwa umakini ili visaidie washiriki kuwa na ufahamu mwema kuhusu changamoto, hali, na maisha ya watu walio na ulemavu.

Kupitia kozi hii, tutakuongozo kwa ufahamu muhimu wa kuwa watu walio na ulemavu ni kama mtu mwingine yeyote, aliye na udhaifu na upungufu, nguvu na sifa, jinsi tulizo nazo mimi na wewe. Vifaa vya mafunzo na shughuli za elimu ya vitendo vya masomo haya zimebuniwa kama zana za kusaidia mshiriki awe na ufahamu mkuu wa kujielewa kwa undani wa binafsi.